Bwana Upepo Wavuma

 


Bwana upepo wavuma! Wimbi lina ghadhabu! Wingu hili linanguruma bandari si karibu,
Hali yetu hufikiri kwa nini kulala? Twafa maji yawe ni karibu wokovu la! Hapana


Refrain
Pepo na mawimbi vyasikia tulia, tulia, kama ukali wa bahari, wanadamu, pepo na shetani
Mawimbi yapataje kuumiza chombo kilicho na Yesu Bwana?
Mambo pia viamsikia tulia, tulia Mambo pia viamsikia tulia, tulia


Bwana nimezima moyo hamu yanizidi tu ninasumbuka roho yangu uniokoe Bwana;
Dhambi nyingi na uovu zitanizamisha Bwana wangu upesi ni wewe utakaenitosha,


Sasa hofu imekwisha ni shwari baharini, Jua letu tena linang’ara utulivu rohoni
Kaa nami ewe Bwana nisiwe mimi tu nami nitafika bandarini ng’ambo niko nafuu

Leave a Reply

Your email address will not be published.