Ukichukuliwa na mashaka yako

 


1. Ukichukuliwa na mashaka yako na kuona
hofu kwamba utakwama,
uhesabu mibaraka yake Mungu ?
na utashangaa kwa rehema yake.


Ref:
Uhesabu mibaraka yote
Mungu aliyoyakubariki !
Ukumbuke mambo yote pia,
na utashangaa kwa rehema yake !


2. Na ukiudhiwa na huzuni nyingi,
ukiona msalaba ni mzito,
Uhesabu mibaraka kuchwa pia,
na kwa moyo wote utasifu Mungu.


3. Wengi watamani mali ya dunia.
utajiri wako ni Mwenyezi Mungu.
Uhesabu mibaraka na kumbuka:
Mali haiwezi kufungua mbingu.


4. Na katika mambo yote huku chini
ukumbuke pendo kubwa la Mwokozi !
Na ujumlishe mibaraka yote,
tena mwisho atakuchukua kwake!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *