Siku ya Mbingu Kujawa Na Sifa
Siku ya Mbinguni kujawa na sifa,
Dhambi zilizidi duniani;
Yesu akaja azaliwe mtu,
Awe na watu ulimwenguni.
Ref
Alinipenda, alinifia,
Ameondoa na dhambi zangu;
Alifufuka nipewe haki,
Yuaja tena Mwokozi wangu.
Na siku moja walikwenda naye,
Wakamkaza msalabani;
Aliumia, aliaibishwa,
Ili atuokoe dhambini.
Siku hiyo wakamlaza chini
Kaburini alipumzika;
Matumaini yetu wenye dhambi,
Ni mwokozi, kwake twaokoka.
Kaburi likashindwa kumshika;
Jiwe likatoka mlangoni,
Alifufuka kwa kushinda kwake,
Naye yuko milele Mbinguni.
Siku moja atatujia tena;
Utukufu wake tutaona;
Atawaleta na wapenzi wetu;
Mwokozi: wangu, tutaonana.