Anisikiaye Aliye Yote
1. Anisikiaye, awaye yote;
Sasa litangaze, wajue wote,
Duniani kote neno wapate,
Atakaye na aje!
Chorus
Ni “Atakaye”, ni “atakaye”,
Pwani hata bara, nalitangazwe;
Ni Baba Mpenzi awaitaye,
Atakaye na aje.
2. Anayenijia, Yesu asema,
Na Asikawie, aje mapema,
Mimi ndimi njia, kweli, uzima;
Atakaye na aje!
3. Atakaye aje, ndiyo ahadi;
Atakaye, kweli ni ya, milele,
Atakaye hilo wote wapate,
Atakaye na aje.