Walio kifoni

 


1. Walio kifoni, nenda waponye,
Uwatoe walio shimoni;
Wanaoanguka uwainue;
Habari njema uwajulishe.


Ref
Walio kifoni waokoeni;
Mwokozi yuko huwangojea.


2. Wajapokawia anangojea,
Awasubiri waje tobani;
Mwokozi hawezi kuwadharau
Huwasamehe tangu zamani.


3. Na ndani ya moyo ya wanadamu,
Huwamo shida, tena huzuni;
Lakini kwa Yesu kuna rehema,
Kuwaponya na kuwaokoa.


4. Walio kifoni, nenda waponye;
Kazi ni yetu, zawadi iko;
Nguvu kuhubiri Bwana hutoa
Kwa subira tuwavute sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *