Umechoka Umesumbuka

 


Umechoka, je, umesumbuka? mwambie Yesu sumbuko lako;
Unayalilia yapitayo? mwambie Yesu pekee.


Refrain
Mwambie Yesu sumbuko lako, yu rafiki amini,
Hakuna rafiki kama yeye, mwambie Yesu pekee.


Je, machozi yakulengalenga? mwambie Yesu sumbuko lako;
Walemewa na dhambi rohoni? mwambie Yesu pekee.


Waogopa shida na majonzi? mwambie Yesu sumbuko lako;
Wasumbukia mambo yajayo? mwambie Yesu pekee.


Kuanzia kifo kukutisha? mwambie Yesu sumbuko lako;
Watamania ufalme wake? mwambie Yesu pekee.

Leave a Reply

Your email address will not be published.