Ni salama rohoni mwangu

 


Nionapo amani kama shwari,
Au nionapo shida;
Kwa hali zote umenijulisha,
Ni salama rohoni mwangu.


Refrain
Salama, Salama,
Rohoni, Rohoni,
Ni salama rohoni mwangu.


Ingawa Shetani atanitesa,
Nitajipa moyo kwani;
Kristo ameona unyonge mwangu,
Amekufa kwa roho yangu.


Dhambi zangu zote, wala si nusu,
huwekwa Msalabani;
Wala sichukui laana yake,
Ni salama rohoni mwangu.


Ee Bwana himiza siku ya kuja,
Panda itakapolia;Utakaposhuka sitaogopa,
Ni salama rohoni mwangu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *