Msalaba Ndio Asili ya mema

 


Sioni haya kwa Bwana,
Kwake nitang’ara!
Mti wake sitakana,
Ni neno imara.


Ref
Msalaba ndio asili ya mema,
Nikatua mzigo hapo;
Nina uzima, furaha daima,
Njoni kafurahini papo.


Kama kiti chake vivyo,
Ni yake ahadi;
Alivyowekewa navyo,
Kamwe, havirudi.


Bwana wangu, tena Mungu,
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu,
Wala kunikana.


Atakiri langu jina,
Mbele za Babaye,
Anipe pahali tena,
Mbinguni nikae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *