Chakutumaini sina

 


1. Cha kutumaini sina,
Ila damu yake Bwana,
Sina wema wa kutosha,
Dhambi zangu kuziosha.


Ref
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye mwamba ni salama,
Ndiye mwamba ni salama.


2. Njia yangu iwe ndefu,
Yeye hunipa wokovu,
Mawimbi yakinipiga,
Nguvu ndizo nanga.


3. Damu yake na sadaka,
Nategemea daima,
Yote chini yakiisha,
Mwokozi atanitosha.


4. Njia yangu iwe ndefu,
Yeye hunipa wokovu
Mawimbi yakinipiga,
nguvu zake ndiyo nanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *