Ninao wimbo mzuri

 


1. Ninao wimbo mzuri, Tangu kuamini;
Wa Mkombozo Mfalme, Tangu kuamini.


Refrain:
Tangu kuamini, Tangu kuamini, Jina lake ‘tasifu,
Tangu kuamini, Nitalisifu jina lake.


2. Kristo anatosha kweli, Tangu kuamini,
Mapenzi yake napenda, Tangu kuamini.


3. Ninalo shuhuda sawa, Tangu kuamini,
Linalofukuza shaka, Tangu kuamini.


4. Ninalo kao tayari, Tangu kuamini,
Nililorithi kwa Yesu, Tangu kuamini.

Leave a Reply

Your email address will not be published.