Chini ya Msalaba

 


1.Chini ya msalaba Nataka simama;
Ndio mwamba safarini, Wa kivuli chema;
Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili,
Tatua mzigo wangu Wakati wa hari.


2.Hapa ni pema sana, Ni ngome kamili;
Hapa yameonekana, Mapenzi ya kweli;
Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani,
Msalaba umekuwa Ngazi ya Mbinguni.


3.Na Yesu msalabani Walimkemea,
Alikufa niokoke Niliyepotea;
Naona ajabu sana Ya mambo mawili
Jinsi alivyonipenda, Nisiyestahili.


4.Atakayeonana, Na Yesu Mbinguni,
Njia yake aanzapo Ni msalabani;
Wokovu upo hapa tu, Mwingine hapana,
Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *